KURASA

Friday, March 26, 2010

JINSI YA KUKATA MICHE YA MISOJI (MITIKI)

Kwa kawaida miche ya misoji mara baada ya kutolewa kwenye kitalu huitaji kukatwa, mjasiliamali aliyeko jijini Mwanza aitwae NAYMA aliniomba nimwelekeze kwa picha na mimi bila hiyana nilikwenda shamba na kung,oa mche mmoja na kuukata na kuupiga picha kabla ya kuukata na baada ya kuukata ili kupata kipandikizi

MCHE KABLA YA KUKATWA (angalia mishale kujua sehemu za kukata)


Mche wangu niliukata na kuacha kiasi cha nchi mbili au pingili mbili za vidole kwa sehemu ya juu ya mzizi na kwenye mzizi niliondoa ile sehemu nyembamba ya chini, kwa kawaida hii sehemu ya chini hufa mara baada ya kupandwa kwa sababu sehemu nene/kubwa ya mzizi inayoachwa ndiyo huifadhi maji na chakula cha mmea, nadhani hapa nitakuwa nimemsaidia kama bado nipigie kwenye ile namba niliyokupa

KIPANDIKIZI TAYARI KWA KUPANDWA


Kumbuka wakati wa kupandwa lazima uweke kisahani ili kiweze kukusanya maji kwa ajili ya ukuaji mzuri, kama ni udongo unaotuamisha maji usiweke kisahani bali wekea kama tuta au mwinuko

WEKA KISAHANI KAMA UDONGO HAUTUAMISHI MAJI


WEKA TUTA KAMA UDONGO UNATUAMISHA MAJI

7 comments:

Anonymous said...

Asante sana kwa kuendelea kutuelimisha, lakini kidogo mimi sijaelewa. Kuna faida gani za kuukata mche wa mtiki kabla ya kuupanda, na je ni lazima kuukata. Ukipandwa hibila kukatwa utakuwaje. Asante sana kwa kuzidi kutufafanulia

Salua said...

Asante kwa kutuelimisha na nimefurahia kupitia blog yako njifunza mengi na napata majibu ya maswalia mengi yaliyokuwa nakosa majibu nitakutafuta tena mbegu zangu zikichipua kwa maelekezi zaidi. Mungu akubariki sana

Bennet said...

Faida ya kwanza ni kupata uhakika wa mche wako kuota kama kutatokea na uhaba wa mvua, kwa kawaida hii sehemu ya juu na ya chuni zinazikatwa hutangulia kufa kama kuna upungufu wa mvua
MAra nyingi huwa tunapanda mara baada ya mvua kuanza, wakati mwingine mvua zinaanza unapanda halafu zinakata hata wiki 4 ndio zinaendelea kunyesha kama kawaida, kama mche wako haujakatwa utakufa kwa sababu sehemu zlizohitaji kukatwa zitatumia akiba yote ya maji, lakini kipandikizi kinauwezo wa kukaa kwenye udongo wiki 4 bila maji na kinaweza kukaa nje ya udongo kwa siku 7 bila kufa

FAida ya pili ni mti wako kunyooka moja kwa moja wakati wa kuota, mara nyingi miche inayoota kwenye vitalu na vipakiti huanza kupinda wakati ikishindana kuota na kutafuta mwanga kwa sababu hulundikwa pamoja, kumbuka zao letu ni mbao na nilazima zinyooke ili ziwe na thamani inayostahili

Anonymous said...

maelezo mazuri

Anonymous said...

Mkuu Bennet,

Huu utirio unao uweka kwenye blogu yako ni muhimu kweli...ubarikiwe.

Soames,
Reading, UK

Tosotwa said...

Hivi wakati wa kupanda miti hii ya mitiki, huwa unatumia mbolea gani?

Tosotwa said...

Hivi wakati wa kupanda miti hii ya mitiki, huwa unatumia mbolea gani?