KURASA

Tuesday, May 4, 2010

JINSI YA KULIMA BUSTANI KWENYE ENEO LENYE MAJIMAJI

Kutokana na tatizo la bwana Chacha Wambura Ng'wanambiti katika post hii hapa http://mataranyirato.blogspot.com/2010/05/aisifuye-mvua-imemnyea.html nimeamua kutoa maelezo kwa ufupi jinsi ya kukabiliana na sehemu ambazo maji husimama wakati wa mvua1- Lima na tifua udongo kwa kutumia trekta la mkono (power tiller) kiasi cha inchi 12 chini, udongo mwingine unaweza kuujaza kama matuta na kuweka mifereji pande zote la eneo lako. Kama huna trekta hili pia unaweza kutumia jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau)

2- Jaza majani makavu, vijiti, maranda ya mbao n.k kiasi cha inchi 5 -6 halafu mbolea vunde au samadi kiasi cha inchi 4 halafu rudishia udongo wako juu yake na hapo utakuwa umeinyajua ardhi yako kiasi cha inchi 8 juu (kumbuka maranda na mbolea vitadidia kidogo) kisha pitisha harrow au jembe la kukokotwa na ng’ombe ili kuweza kuchanganya vitu hivi3- Acha udongo wako ukauke kiasi cha siku 3 kisha pitisha harrow au jembe la kukokotwa na ng’ombe tena ili kuvunja vunja mabonge ya udongo yaliyotokea wakati wa udongo kukauka na pia kuchanganya mchanganyiko huu zaidi

4- Weka tena mbolea vunde au samadi kiasi cha nchi mbili juu ya mchanganyiko huu kisha panda mbegu au miche yako na uizungushie udongo kiasi

5- Mwagia maji kadri inavyo hitajika kama udongo utakuwa mkavu, na uendelee kufuata kanuni za kilimo bora kama inavyoshauriwa kitaalamu

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe lijamaa inaonekana ni litaalamu la haya madude ya kilimoz ehe?? itabidi nilitafute kwanza

Elyc said...

Kaka mie naomba unielekeze jisi ya kuprune mimea aina ya michungwa na milimao ile ya ku-bud.naenda shamba jumamosi nimepanga ndio iwe siku maalum kwa ajili ya shughuli hiyo nina mimea kama 300 na zaidi niliipanda mwaka jana sasa naona mingine inarefuka sana na mingine kama imedumaa yaani hata sielewi.Please help