KURASA

Sunday, August 15, 2010

KILIMO CHA MICHUNGWA NA MACHENZA

Ndugu Ali Kalufya alitaka kujua kwa kina ukuliama wa michungwa na jamii yake, aliuliza swali hili katika mtandao wa Dada Subi nami najaribu kumweleza haya...

Michungwa na Jamii yake hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye joto kiasi, mvua nyingi na udongo wenye rutuba, kwa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki

MBEGU
Kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kisha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.

KITALU
Mwaga mbegu zako kwenye kitali na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimeta, mwagia maji kilasiku na baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kuchipua,

MICHE YA MILIMAO TAYARI KWA KUUNGWA


baada miche kufikia kiasi cha sentimeta 3 - 5, miche ihamishiwe kwenye pakiti zenye udongo wenye mbolea ya kutosha na viwekwe kwenye kivuli kiasi

MICHE YA JAFFER BAADA YA KUUNGWA


KUUNGA MICHE
Miche ikifikia urefu wastani sentimeta 30 - 45 inawezwa kuungwa ikiwa unataka iwe michungwa au michenza, kazi hii inahitaji utaalamu kiasi na unaweza kuomba msaada kutoka kwa maafisa ugani wa Kilimo. Kwa michungwa kuna iana mbili kuu hapa Tanzania ambazo ni Jaffer na Valencia. Jaffer ni rahisi kuunga kwa sababu vikonyo vyake ni vikuwa na viko wazi kwenye miti,miti yake huwa mikubwa na inazaa sana, lakini huathirika sana jua likiwa kali na matun da mengi huanguka, pia machungwa yake hukua na kuiva haraka, soko likiwa baya mengi huishia shambani kwa kuanguka

MTI WA JAFFER


JINSI YA KUUNGA MICHE YA MILIMAO KUWA MICHUNGWA AU MACHENZA


Valencia ni miti ya wastani, vikonyo havipo wazi kwa hiyo huwapa kazi waungaji (hawaipendi) ina uzao wa wastani na inakabili ukame na matunda yake hayaivi haraka, msimu wa machungwa ukiwa katikati wewe ndio unaanza kuvuna na ukisha bado unakuwa na machungwa wakati bei iko juu

MTI WA VALENCIA



UPANDAJI
Baada ya uungaji kukubali unaweza kuandaa shamba lako kwa kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kusubiri msimu wa mvua, miche ipandwe mara baada tu ya mvua za kwanza kunyesha, umbali wa kupanda ni mita 8 * 8 kwa jaffer na mita 5 * 8 kwa valencia

KUPALILIA
Miche isafishiwe si chini ya mara 2 - 4 kwa mwaka na miche ikifikisha miaka mitatu unaweza ukasafishia visahani na kufyeka sehemu nyingine

UZAO
Kuanzia miaka mitatu miche itaanza kutoa maua na kuzaa na huchanganya kuzaa baada ya miaka mitano, miche huendelela kuzaa hadi kufikia miaka 25 - 30 tangu kupandwa

WADUDU/MAGONJWA
Magonjwa makuu ni fangasi, miti kunyauka na nzi wa michungwa, dawa kwa ajili ya magonjwa yote haya zinapatikana madukani

CHUNGWA LILILOSHAMBULIWA NA NZI WA MICHUNGWA

19 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka! siku nyingi sijakuona wala kukusikia sijui kwa vile nami nilikuwa likizo? Ahsante sana kwa hili somo kwani nimepanda michungwa ruhuwiko lakini naomba kuuliza miche ya michenza inapatikana wapi kwani nimetafuta na sijapata pia matunda damu (tamalilo)

Bennet said...

Samahini kwa kupotea kwenye kijiwe changu kwa muda, nilikuwa nipo Tanga navuna mahindi na pia huu ni msimu wa machungwa kwa hiyo nilikuwa nasimamia mavuno na mauzo, pia nilikwenda Morogoro na Singida kujifunza vitu fulani

Kwa miti ya michenza ni vizuri kama utatumia kuunga kama nilivyoeleza kwenye somo langu, ingawa miche inapatikana SUA na TTSA, kuhusu matunda damu ngoja nikuulizier kwanza

John Mwaipopo said...

mzee kweli ilibaki kidogo tukutangaze 'amepotea'. masomo yako nayafurahia sana. karibu

Anonymous said...

Hongera Ndugu Bennet kwa ushauri wako mzuri
Naona mti wa jaffer ni mkubwa kuliko valensia na mti wa jaffer umezaaa sana na pia umeangusha sana matunda
SWALI je miti hii ilipandwa pamoja yaani na umri sawa? je picha hizo zilipigwa siku moja?

Anonymous said...

Mtaalamu kama ulikuwa unavuna mahindi kwanini basi usituwekee ukulima bora wa mahindi kwa sababu hiki ndio chakula chetu kikubwa wabongo

Bennet said...

Anony wa kwanza ni kweli kwamba mti wa jaffer na valancia imependwa siku mija na ina umri sawa, ukianagalia utaona kwamba jaffer ni mkubwa sana na umezaa sana lakini pia yameangua wakati kwenye mti wa valancia machungwa ndio yana komaa

Anony wa pili nimeshaweka maelezo ya kilimo cha mahindi, nilipanda mahindi ekari 3 ambapo kuna michungwa midogo na nikavuna magunia 95 yaani kilo 95,000

Anonymous said...

Je katika kilimo cha mahindi ulitumia mbegu gani hiyo uliyopata mavuno hayo

Ney said...

Bennet nimevuna machungwa yangu. Yamepamba sana machungwa ni mengi lakini kuna mti mmoja kila chungwa lina doa moja kubwa na ukilikata unakuta lile doa liko mpaka ndani ya chungea na linasababisah chungwa kuoza je nifanyeje?
Nayma

icecream sandwich said...

nataka kulima machungwa,vipi uhakika wa soko,ntauza wapi?

Unknown said...

Hi salama ndg!Natafuta sehemu nitakayo pata begu ya limao!

Unknown said...

Nahitaji miche iliyofanyiwa buding nipo iringa

Unknown said...

Nahitaji miti iliyofanyiwa budding /grafting. Inauzwaje na itachukua muda gani iwapo nikiipanda kipindi hiki mpaka ntakapoaanza kuvuna. Nipo kigoma.

Unknown said...

Hatua za kuotesha machungwa ni sawa na hatua za kuotesha malimao na machenza?

Unknown said...

Chacha

Unknown said...

Habar mtalaamu!!?
Naomba kujua aina za machenza kama zipo

Unknown said...

Nahitaji mbegu za machenza limao na machungwa nitazipata wapo

Unknown said...

kaka habari, nina ekari 10 bungu. Huwa naona machugwa yanakubali sana. Sema kule ardhi iko vizuri sana kiasi ya kwamba wa2 hawawekii mbolea.

Unknown said...

je bungu ni sehemu sahihi kwa kilimo hicho??

RAS ERIC said...

Mbona hauelezei kwa kina juu ya magonjwa na aina ya mdawa? Ivi hujui hivyo ndivyo vipengele muhimu sana ktk tija ya zao husika?