KURASA

Friday, January 7, 2011

UJERUMANI KATIKA KASHFA YA SUMU AINA YA DIOXINE

Nchi ya Ujerumani imeeingia katika kashfa baada ya mayai na kuku kukutwa na kirutubishi ambacho ni sumu aina ya dioxine ndani yake, inaaminika kwamba kirutubishi hicho kilisambazwa kati ya mwezi Novemba na Disemba mwaka jana kwa kampuni 25 za kutengeneza vyakula vya mifugo.Sumu hiyo iligundulika katika majimbo 7 nchini Ujerumani wiki iliyopita, lakini wiki hii kimegundulika nchini Uholanzi ambapo Ujerumani iliwauzia mayai na kuku walioathiriwa na sumu hiyo.

Kiasi cha mayai 136,000 (toka kampuni mbali mbali za kuzalisha mayai )tayari yamegundulika kuwa na sumu hiyo, sumu hiyo iliingizwa katika virutubishi chakula (concentrates) kiasi cha tani 3000 ambazo zilinunuliwa na kutumiwa na makampuni mbali mbali.mayai na kuku wote wenye sumu hiyo wakizuiliwa kuuzwa kwa matumizi yz Binadamu, Uchunguzi unaendelea ilikujua kama sumu hiyo ipo kwenye mazao menine ya mifugo kama nyama za ng;ombe na nguruwe, maziwa n.k

1 comment:

maisha ni mikikimikiki said...

HII SASA SHIDA KWA WALAJI WA NYAMA NA MAYAI YA KUKU.
HAPA NIPENI ELIMU YA UTUNZAJI WA KUKU WA KIENYEJI KWA KUTAJA AINA ZA VYAKULA VYA KUKUZIA VIFARANGA WA KIENYEJI NA DAWA ZA KUZUIA MAGONJWA.