KURASA

Wednesday, April 6, 2011

SALAMU TOKA KWA MELTON KALINGA - MOROGORO

Wanachuo toka SUA wakipata maelezo toka kwa Bw Kalinga walipotembelea kituo cha utafiti na uzalishaji samaki Kingolwira Morogoro



Vifaranga wa sato wakiwa tayari kwa kupandikizwa kwenye bwawa



Uvunaji wa sato toka kwenye matanki ya kujengea na saruji eneo la Kingolwira


Sato waliokwisha vuliwa tayari kwa kuwa kitoweo


Kambale jike mwenye mayai tayari kwa ajili ya kufanya upandishaji na mbegu za dume kwa njia bandia ambao hufanyika nje ya mwili wa samaki hawa kwa kutumia mtambo maalum (rejea makala zangu)


Ndugu Melton Kalinga ni mtaalam wa ufugaji wa samaki toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anapatikana Morogoro Kwa mawasiliano zaidi mpigie kupitia 0757891761 au 0787596798 ili kupata maelezo kama ya ufugaji bora wa samaki, namna ya kupata vifaranga vya samaki anavyo zalisha, jinsi ya kulisha samaki wako, uchimbaji na ujenzi wa mabwawa n.k

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha kuona umerudi kuwa nasi kaka Bennet, Tulikuwa na wasiwasi kuwa umepotelea wapi? Na asante sana kwa soma hili la samaki...umenikumbusha zamani kaka zangu walichimba kisima na tulikuwa tunafuga samaki walikuwa watamu kweli ngoja niwape wazo hili wachimbe tena....

Anonymous said...

kaka ben twashukuru umerudi kwani tunahitaji mchango wako jee inawezekana kukutembeleya kazini kwako ili tuweze kuuliza na kupatiwa maelezo yanayohusiana na pirika zetu za kilimo na ufugaji jee tunaweza kutumiya njiya gani?ili kukuona na kupata maelekezo tunayohitaji .

Anonymous said...

Brother Ben nimekumiss saaanaaa binafsi, nafurahi sana kwa kurudi kwako. TAFADHALI USIJICHIMBIE TENA INGAWA NAJUA MAJUKUMU YAMEONGEZEKA HASWA BAADA YA KUOA, MWAMBIE SHEM HATA SISI TUNAUHITAJI UTAALAAM WAKO MKUBWA WA KILIMO.

Nayma said...

Kaka Ben Usipotee sana hapa tunajifunza mengi kupitia hapa

Thomas Ludovick said...

Kaka hivi hii idea uliitolea wapi?na uliwaza nini?wakati ukiwa umelala muda huo.Kiukweli i see that ur veru creative person ambae unaweza kufanya kitu fulani katika TANZANIA hii iliyojaa kila aina ya mambo. Kilimo, ufugaji ndio kitu muhimu sana katika maisha ya sasa.Nimepitia leo blog yako nimejonea mengi sana nimejifunza jambo hapa pale kwetu naweza kuanzisha Garden na nikalima.Nyie ndio watu mnaotakiwa katika masuala kama haya ili kutoa elimu naona umepiga hatua kubwa sana.Fanya kazi yako kwa bidii achana na mfumo wa ufisadi hapa Tz.Fanya jambo kwa mantiki na kwa kufikiri pia utafanikiwa.Tangu mwanzo nilikuwa nasema Tanzania watu wenye kila uwezo wa utalaamu wapo tatizo tunashindwa kuwatumia hapa tunabaki kupiga kelele na mafisadi hawatuusu cha msingi ni kufanya kazi kwa bidii kama wewe.Ila hapa changamoto ninayoiona je, hivi watu wa vijijini wanapata kweli hizi taarifa maana kule hakuna access ya internet je, watajuaje haya mambo au una program yoyote unayoifanya kuwafikia watu waliopo vijijini...Aksante na Mungu akubairiki kwa moyo huo mafanikio yawe juu yako. Kazi ndio uti wa mgongo sio kilimo kama kama wanavyosema 'Ninasema ni ardhi kwanza na sio kilimo kwanza bila ardhi kilimo hakuna'