KURASA

Tuesday, August 28, 2012

CANINE PARVOVIRUS

Kama jina lake lilivyo ungonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo huwaathiri mbwa ka kiasi kikubwa, ugonjwa huu uligundulika miaka ya 1970 na hushambulia zaid seli za kwenye mfumo wa chakula na hewa. virusi vya ugonjwa huu huwa vingi sana kwenye kinyesi cha mbwa mgonjwa na  husambaa baada ya mbwa kugusa kinyesi che nye vidudu kwa mdomo wake, huweza pia kubeba virusi hivi kama atavilalia au kukanyaga kinyesi cha mbwa mwenye ugonjwa huu, na mbwa anaweza pia kuambukizwa ikiwa atagusa kitu chochote ambacho kiligusana na kinyesi chenye vidudu vya parvo.


DOBERMAN PINSCHER

Ugonjwa hushambulia mbwa wa umri wowote lakini watoto wenye umri kati ya wiki 6 - 20 hushambuliwa zaidi na pia mbwa aina ya Doberman Pinschers and Rottweilers hushambuliwa zaidi ya mbwa wengine ha dalili za ugonjwa huu huonekana kirahisi kwao.


ROTTWEILER

Dalili za kwanza huonekana baada ya siku kama 5 ambazo ni kuharisha, kutapika na joto kupanda sana ingawa si mbwa wote ambao watapandisha joto, watoto wataonyesha dalili za kusumbuliwa na maumivu ya tumbo, pia kinyesi hutoka na malenda malenda ambayo wakati mwingine huwa na damu damu kiasi na kwa wataalamu wa mifugo kipimo cha ELISA huweza kutumika kupima na kugundua virusi vya ugnjwa huu

MATIBABU
Hakuna matibabu ya ugonjwa huu ila drip za maji husaidia kurudisha maji yaliyopotea na kumpa nafuu mgonjwa, dawa za kuzuia kuharisha na kutapika ni muhimu na pia wakati mwingine mbwa anaweza kuhitaji kuongezewa damu, antibaiotiks pia ni muhimu kuzuia maambukizi ya bakteria

Kupona kwa mbwa kutategemea vitu vingi kama ukoo wa virusi vya ugonjwa, hatua za maambukizi, uwezo wa mwili wa mbwa kupambana na magonjwa na umri wa mbwa hata uharaka wa kuapata tiba kwa mbwa

KINGA
Kinga kubwa ni chanjo ya DHPP (distemper, hepatitis, parvovirus, and parainfluenza combination)ambayo hupigwa katika umri wa wiki 8 tangu kuzaliwa na kurudiwa baada ya wiki 16 lakini kama wazazi hawakuchanjwa basi ni muhimu kuchanja katika wiki ya 4, usafi wa mabanda pia ni muhimu lakini ukitumia blichi kiasi cha 1:30 katika uchanganyaji na maji ukisafisha na kuiacha kwa zaidi ya dakika 20 kabla ya kuiosha na maji

2 comments:

emu-three said...

Mkuu twashukuru sana kwa shule hii,tupo pamoja

Bennet said...

Aksante na karibu sana