KURASA

Wednesday, August 15, 2012

SUKUMA VUTA -Njia bora ya kupambana na kiwavi mshambulia mabua ya mahindi (maize stalk borer)


Kiwavi anayeshambulia mabua ya mahindi anajulikana pia kama maize stalk borer (Sesamia fusca) kiwavi huyu hutokana na vipepeo weupe wanao onekana kwenye mashamba ya mahindi, vipepeo hawa hutaga na baada ya mayai yao kuanguliwa ndipo viwavi hawa waharibifu hutokea na kuanza kushambulia mahindi shambani



Viwavi hawa hushambulia katikati ya mabua na kusababisha mmea kudumaa na kisha kufa, hali huwa mbaya zaidi kama mashambulizi yatatokea wakati mimea ikiwa bado michanga maana mkulima hatavuna kabisa katika mimea iliyoshambuliwa na pia hupunguza mavuno kwenye mimea iliyokomaa na kutoa mbelewele



Njia hii ya sukuma vuta ni njia yenye mafanikio kwa asilimia kupambana na viwavi hawa kama utafuata maelekezo kwa usahihi, na hii itakusaidia kupambana na viwavi hawa kwa njia ya kibaiolojia bila kutumia kemikali zozote shambani mwako
 Ilikupambana na viwavi hawa waharibifu kwenye shamba lako la mahindi, panda mimea ya desmodium kila baada ya mistari mitano ya mahindi, desmodiuM husaidia kufukuza vipepeo na viwavi kutokana na harufu yake kali na wakati huo huo kuongeza nitrjeni kwenye udongo shambani

Panda majani aina ya napier kuzunguka shamba lako, kwani majani haya huwavutia pia vipepeo na viwavi hawa waharibifu, wakati desmodium inawafukuza nje ya shamba lako viwavi hawa, majani ya napier yanakuwa yanawavuta nje ya shamba lako na ndio maana njia hii ya kibaiolojia hiutwa SUKUMA VUTA

No comments: