Unaweza kupanda kwa kutumia mbegu au kwa kununua miche bora kutoka kwenye taasisiza kilimo mfano Uyole Mbeya. kama utatumia mbegu basi ni bora kununua mbegu bora au ukikosa mbegu basi jaribu kutumia zile utakazopata kutoka kwenye tunda lenyewe
Kama utachukua za kwenye tunda basi zikaushe kwenye jua kwanza mpaka zikauke kabisa, zile za kukununua huwa zimekauka kwa hiyo huna haja ya kuzikausha, Chukua karatasi laini (napkins/tissues) iloweshe maji kiasi kidogo kisha chukua mbegu zako na uzifunge na karatasi hii vizuri kisha ziwekw kwenye jokofu kwa kiasi cha wiki 3-4 zitaanza kuota/kumea, kuziweka kwenye friji husaidia kuua vijidudu vya magonjwa ambavyo huenda vilikuwepo kwenye tunda au mbegu
Chukua mbegu yako na uipande kwenye mifuko au chombo kama ndoo, usipande kwenye vifuko vidogo maana mmea huu hukua mkubwa kiasi na wenye mizizi mikubwa kabla ya kupandwa. Mmea wako ukifikia ukubwa wa futi moja mpaka pili ni kipindi kizuri kuuhamishia shambani,
Umbali wa shimo hadi shimo ni kiasi cha futi 15 mpaka 18 kutoka mti hadi mti. Hakikisha unapanda miche yako wakati wa mvua za kwanza, Mashimo yawe na kina cha futi mbili na upana futi 3. Weka kasi cha debe 1 la samadi au mboji na changanya vizuri na udongo.
kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanya maji ya mvua au unapomwagilia na utandaze majani/nyasi kiasi cha futi 3 kuzunguka mti wako, hakikisha wanyama kama mbuzi na ng'ombe hawaingii shambani na kula miti yako. Baada ya mwaka hutakuwa tena na haja ya kumwagilia miti yako kwani itaweza kukua yenyewe kwa kutegemea mvua
WADUDU NA MAGONJWA
Wadudu wanaoshambulia zaidi mitufaa ni vidukari (moth) na pia ugonjwa wa madoa meusi (black spot) ndio unaoshambulia zaidi, ili kupambana na ugonjwa na wadudu hawa hakikisha unatuma kiutilifu chochote che nye pareto (pyrethrum) ndani yake
Uvunaji ni baada ya miaka mitatu lakini miche ya kuunga huanza kuzaa mapema hata ndani ya mwaka, ila nashauri usiruhusu matunda mengi kwenye miti midogo ili kuzuia matawi kuvunjika kwa hiyo punguza matunda kabla hayajawa makubwa na kubakisha machache
7 comments:
Nilikuwa sijui kama Songea inawezekana....ngpja nibaribu maana matamu sana
Ni kweli Dada Yasinta haya matufaa yanastawi sana sehemu zenye ubaridi
naomba kuuliza je naweza fanya kilimo cha matufaa kwenye kitalu nyumba?kama inawezekana naomba kujua specification za space
Tarime inawezekana pia au siyo?
sujaelewa kuhusu kuzipanda mpaka ziote hizo matufaa
Nzuri kuna niche ipo kwa anae hitaji
Post a Comment