KURASA

Friday, March 28, 2014

TOGGENBURG - AINA BORA YA MBUZI WA MAZIWA


Hii ni aina ya mbuzi wa maziwa ambao asili yake ni uswizi katika eneo la Obertoggenburg kama wanavyoitwa, hii ndio mbegu ya mbuzi wa maziwa wa zamani zaidi kuliko zote. Kwa hapa Tanzania wanapatikana Uyole, SUA na Tengeru (hivi vyote ni vyuo vya mifugo)

UZALISHAJI
Mbuzi hawa wanauwezo wa kuzalisha maziwa wastani wa lita mbili kwa siku au zaidi, hawatoi maziwa mengi kama Saanen ila maziwa yao yana kiasi cha mafuta kati ya 3% - 4%

MAUMBILE
Mbuzi hawa wana umbile la wastani lakini ni wakubwa kuliko mbuzi wa kienyeji, kilo 55 kwa majike na kilo 75 kwa madume, wana rangi ya kahawia (khaki) mpaka hudhurungi (brown)  pia wana mistari miwili usni yenye rangi ya maziwa au nyeupe kuanzia juu mpaka kwenye pua (kama duma) huwa na viwele (udder) vikubwa na pia ni wazazi na walezi wazuri, mara nyingi huweza kuzaa mapacha 

HALI YA HEWA
Mbuzi hawa hawawezi kuhimili hali ya joto, bali hufanya vizuri kwenye maeneo yanye baridi kama mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe, Dodoma, Singida n.k. Wanahitaji chakula chakutosha ili kutoa maziwa mengi, pia chakula kiwe na virutubisho kamili. Ingawa pia wanaweza kuchungwa kwenye maeneo yenye ukame kiasi na wakaweza kufanya vizuri (good foragers)

TABIA
Mbuzi hawa huishi kwa makundi wakitoroka au kuingia kwenye shamba la mazao basi huenda wote na hufundishika kirahisi sana hii husababisha urahisi wa kuwafundisha kukamuliwa na mashine

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa dasara kakangu!!

mohamedi rasuli said...

Vp hali ya hewa ya tanga hao mbuzi wanaweza kuishi nakuzaliana kama kawaida

mohamedi rasuli said...

Vp hali ya hewa ya tanga hao mbuzi wanaweza kuishi nakuzaliana kama kawaida

Bennet said...

Tanga kuna hali za hewa kama tatu, maeneo ya Lushoto ni baridi mbuzi hawa wataishi vizuri, maeneo ya Amani, Kuze, Daluni ni wastani mbuzi hawa pia yatawafaa, ila huku pwani kwenye joto hawata kubali sana labda uwachanganye na wakienyeji kupata chotara

Miradi Kwanza said...

ahsantevipi kuhusu soko la maziwa ya mbuzi kuu.

Edward GAS said...

Nahitaji kununua mbuzi wa maziwa aina ya Saanen kama wanne hivi pamoja na mbuzi aina ya togenberg kama wanne hivi pamoja na madume yao hata moja moja,Is how much na je nitwapata wapi?

Edward GAS said...

my phone numbers are +255 784 707 352 na +255 767 707 352