KURASA

Tuesday, July 12, 2016

AGRI-HUB TANZANIA

Agri-Hub Tanzania ilizinduliwa rasmi Oktoba 2012. Uzinduzi huo ulikuwa tukio lenye maana kubwa kwa wote waliokuwepo, ikizingatiwa kwamba ipo haja kubwa ya kushrikiana na kuunganisha juhudi katika uimarishaji wa kilimo. Serikali ilifurahishwa na hatua hii ambayo pia iliungwa mkono na sekta binafsi, jumuiya za wakulima na asasi za kijamii. Wanachama wa Agri-Hub wameunda vikundi-kazi 5 ambavyo vitakuwa na shughuli zifuatazo: uhamasishaji, mafunzo, kuratibu utendaji na mbinu za kibunifu kwa lengo la kuimarisha uzalishaji endelevu wa chakula na kuboresha maisha ya wakulima wa Mkoa wa Arusha.


Shughuli za awali

Kundi la uchanganuzi lililopendekezwa na wanachama kadhaa wa Agri-ProFocus na wadau wengine nchini lilileta msukumo uliowezesha kuanzishwa Agri-Hub Tanzania. Hadi kufikia sasa, tayari jumuiya zipatazo 25 zimeshajiunga na taasisi hii, ikiwa ni pamoja na: SNV, RijkZwaan, TRIAS, Cordaid, Hivos, Agriterra, Farm Africa na Faida Mali. Taasisi zote zina dhamira moja: kuunga mkono shughuli za Agri-Hub Tanzania kwa kujitolea kwa hali na mali katika kuendeleza Agri-Hub. Arusha, jiji lililo kaskazini mwa Tanzania ambalo lina umuhimu mkubwa katika shughuli za kilimo likiwa pia ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), liliteuliwa kuwa makao makuu anzilishi ya Agri-Hub.

Upangaji wa agenda: Warsha wa wadau wa sekta mbalimbali

Hafla ya kikazi iliyofanyika tarehe 5, Oktoba ilitayarishwa kwa lengo la kuwaarifu wadau wa kilimo na wengineo wenye ushirika na kilimo katika Mkoa wa Arusha, juu ya mikakati iliyokuwa ikitayarishwa na pia, juu ya warsha wa mipango.

Warsha wa Wadau wa Sekta Mbalimbali (22 – 23 Oktoba, 2012) ilitoa fursa kwa wanachama wa Agri-Hub kupanga Agenda.

Wakati wa warsha, wanachama waliunda vikundi-kazi vifuatavyo:

- Upatikanaji wa Ardhi

- Upatikanaji wa Mitaji

- Upatikanaji wa Pembejeo

- Upatikanaji wa Masoko

- Mtazamo wa Kibiashara kwa Wakulima

Upatikanaji wa ardhi

Ijapokuwa sheria za Tanzania zinatambua haki ya wakulima wadogo kumiliki ardhi na kufanya shughuli za kilimo kwenye ardhi hiyo, wakazi wengi wa vijijini hawajaelimishwa juu ya manufaa mengi wawezayo kuyapata kutokana na ardhi yao.

Kikundi-kazi hiki kina lengo la kuboresha hali ya wakulima kwa kuwapa mafunzo na wadau wengine wa ardhi jinsi ya kutumia kwa manufaaa yao Sheria za Ardhi zilizopo.

Upatikanaji wa mitaji

Huduma za kifedha kwa wakulima ni suala muhimu kwa jamii inayotegemea kilimo kama Tanzania. Kikundi-kazi cha mitaji kimetayarisha mlolongo wa shughuli kwa minajili ya kuunga mkono harakati za utafutaji wa mitaji kwa miaka mingi ijayo. Kikundi hiki kinatazamia kupanga na kujenga ushirikiano na mikakati ambayo tayari ipo (kama vile like Maonyesho ya Kilimo-Biashara, nk) kwa lengo la kuongeza utelekelezaji na utendaji wa kiwango cha juu iwezekanavyo.

Upatikanaji wa Pembejeo

Kulingana na mtazamo wa kikundi-kazi cha pembejeo, upatikanaji na uwepo wa taarifa kamili juu ya pembejeo ni jukumu la pamoja la wakulaima, makampuni mbalimbali na serikali.

Kikundi hiki kimetayarisha shughuli mbalimbali zenye lengo la kuunganisha hawa wadau wote ili waweze kufikia lengo hili:kuwaelekeza wakulima wajue ni wapi pa kupatia pembejeo na waweze kufanya uteuzi sahihi wa pembejeo hizo na jinsi ya kuzitumia.

Upatikanaji wa Masoko

Maudhui ya kipengele hiki yanajumuisha maudhui mengine kadhaa madogovidogo, kama vile: Mfumo wa taarifa za masoko, kukutana na wanunuzi, kilimo cha mkataba na mengineyo. Hatua inayofuata ni kuangalia ni nini ambacho kila mwanachama wa kikundi-kazi anaweza kuchangia katika majadiliano. Aidha, kunakuwepo na uchunguzi kuona ni jumuiya gani ambazo zingepaswa kuhusishwa lakini bado hazipo, ili ziweze kuunaginshwa na Agri-Hub.

Mtazamo wa kijasiriamali kwa wakulima

Kujengea wakulima mtazamo wa kijasiriamali ndio lengo kuu la Agri-ProFocus. Lakini je, ni kwa vipi tutaweza kutekeleza azma hii katika kiwango cha kimkoa? Kikundi-kazi hiki kinalenga kuwahamasisha wakulima wenye upeo wa juu kuliko wenzao, waweze kuthibitisha wazi kuwa kilimo biashara yenye tija kama biashara zingine, iwapo itaendeshwa kwa njia sahihi.

Je, ungependa kujiunga?

Shughuli za Agri-Hub zimo katika matayarisho na utekelezaji wake utaanza hivi karibuni. Iwapo una nia ya kuingiza mada yako katika agenda, basi jiunge na vikunndi-kazi vilivyoorodheshwa hapo juu mapema iwezekanavyo. Agri-Hub Tanzania itakuwezesha kupata washirika ambao, kwa kujiunga nao, utaweza kufanikiwa katika malengo yako!

Kwa maelezo zaidi:

Apollo Muyanja Mbazzira (SNV)

Mratibu wa Agri-Hub Tanzania

Baruapepe: amuyanja.agrihub@gmail.com

Simu: +255 22 260 0340

Marjolein de Bruin

Mwezeshaji mtandao: mdebruin@agri-profocus.nl

Simu: +31 (0)26 3542056

Jiunge na jukwaa la Intaneti:

http://apf-tanzania.ning.com/   Agri-Hub Tanzania, Plot 1124, Chole Road, Msasani Peninsular, P.O. Box 3941, Dar es Salaam, Tanzania

Agri-ProFocus, Willemsplein 43-II / P.O. Box 108 – 6800 AC ARNHEM (NL)

T: +31 (0)26 354 2074 / E: info@agri-profocus.nl / www.agri-profocus.nl

No comments: