KURASA

Monday, February 16, 2009

ALOE VERA - KINGA YA MALARIA


Sina uhakika na jina halisi la mme huu wengi wanauita SHUBIRI au SHUBIRI MWITU wengine huiita LITEMBWE (nafikiri ni jina la kiluga) kuna makala kadhaa zinasema shubiri ni mti kamili na wala si mmea, kama yuko ambaye anajua kwa uhakika naomba atusaidie.

Naomba mkumbuke kwamba kila ninachoandika humu ni kwamba nimehakikisha ukweli wake labda kwa kuona au kutumia mimi mwenyewe na wala sijasoma sehemu na kisha kuandika humu.

Nitaongelea kuhusu Aloe vera kama kinga ya malaria, kwa sababu mimi mwenyewe nilisha wahi kuwaandalia watu hii dawa na ikawasaidia, kwa mfano kuna ndugu yangu mmoja alikuwa anaumwa na malaria kila baada ya miezi 2 - 3. nilimpa hii dawa dozi moja tu na aliweza kukaa miezi 14 (mpaka leo hii)bila kuumwa malaria

Inasemekena kwamba mmea huu unauwezo wa kutibu magonjwa mengi kama vidonda, muwasho wa ngozi na harara, husaidia kusaga chakula, hupunguza uvimbe, hupunguza kiasi cha lehemu (cholestrol) mwilini na mengineyo


Huu ni mmea maarufu sana duniani kutokana na kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi, na pia unapatikana sehemu nyingi za dunia hasa zile ambazo hazina baridi. Vipodozi vingi vya ngozi vinachanganywa na mmea huu ili kuvipa uwezo zaidi wa kutunza ngozi


Mmea huu unatumika zaidi kama majani ingawa shina na mizizi yake nayo ni dawa pia, mmea huu huwa na umbo la kama katani/mkonge au mmea wa nanasi ila wenyewe ni mdogo kidogo na huwa laini zaidi


Majani yake yana sehemu mbili, kuna ganda la nje na maji ya ndani (jelly) ganda la nje lina kemikali za kutibu zaidi na ule utando wa ndani una virutubusho vingi sana ambavyo ni kinga za mwili


KINGA YA MALARIA
Kama unasumbuliwa na homa ya malaria mara kwa mara, chukua majani mawili yaliyo komaa, yaoshe vizuri na kata kata katika vipande vidogo.


Changanya na maji vugu vugu kisha saga kwa kutumia kisagio (blender) au twanga kwenye kinu kidogo, chuja na kisha ongeza maji hadi upate bilauri (jug) nzima, unaweza kuhifadhi dawa hii kwenye friji MATUMIZI kunywa vikombe viwili mpaka vitatu kwa kila siku kwa siku 5 - 7. Hii itakusaidia kuongeza kinga ya mwili wako maradufu na unaweza kurudia dozi hii mara baadda ya miezi 3 - 4.

8 comments:

Mbele said...

Bora umekuja tena na somo jingine, baada ya siku nyingi kidogo. Ni kweli huu mmea unathaminiwa kama dawa sehemu mbali mbali katika nchi yetu, na kwingineko. Shukrani, na kila la heri.

Subi Nukta said...

Shukrani kwa kutoa dozi ya Malaria, sasa mjomba wangu anayesumbuliwa na malaria sugu inayojirudia kila baada ya miezi mitatu pamoja na kutumia kila aina ya dawa ya malaria aliyowahi kuambiwa, hii itabidi aifuate kama ulivyoiandika.
Kweli uzuri na faida ya elimu ni kushirikisha wengine.
Asante sana Bennet!

Yasinta Ngonyani said...

Haya kaka Bennet sasa nimeona na nasema Asante sana kwa mafunzo yako ya elimu hii

Bennet said...

Dada Yasinta endelea kupita humu ili upate elimu kidogo niliyo nayo ambayo nina uhakika na wewe utawaelewesha wengine kwa manufaa ya watu wote

ukija dsm tuwasiliane niweze kukupa mche mmoja wa aloe vera kama zawadi

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante Bennet ntafanya hivyo. Na usiwe na shaka ntakuwa napita kila siku kwani kuna elimu safi sana

Anonymous said...

Asante sana kaka Rhxoqsa kwa kutuelimisha,,,mimi nasumbuliwa sana na maralia mara kwa mara sasa nikirudi Tz itabidi nitumie hii dawa
baraka

faustamairia said...

NAMI NASHUKURU SANA KWA KUWA NASUMBULIWA NA MALARIA SANA NA ALOE VERA NINAYO NIMEPANDA LAKINI TATIZO KUBWA LILIKUWA KIPIMO CHA KUTUMIA. LAKINI JE NI KWELI UKITUMIA NYINGI UNADHURIKA? MIMI HILO PIA LILINIOGOPESHA KWA HIYO NIKAOGOPA KUTUMIA.

Unknown said...

Shukrani kwa somo