KURASA

Sunday, March 29, 2009

MKUYU

MTI WA MKUYU



Huu ni mti unaopatikana sehemu nyingi sana duniani kuanzia ukanda wa joto mpaka nyanda za juu zenye baridi, ni mti ambao unakuwa na majani kipindi chote cha mwaka (evergreen) sehemu unazopenda kuota ni mabondeni na hasa sehemu chepechepe ingawa mara nyingine hupatikana hata sehemu ambazo si za majimaji sana.


SHINA NA MAUA/MBEGU




Mti huu unasifika sana kwa sifa ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kama una kisima cha msimu ambacho hukauka maji kipindi cha jua kali basi panda mti huu karibu na kisima. Mti utakapo kuwa na ukubwa wa wastani kisima chako kitakuwa na maji mwaka mzima, mizizi yake ambayo hutambaa sana huifadhi maji ardhini yasichukuliwe kama mvuke wakati wa jua kali na pia kivuli cha majani yake pia husaidia kutunza maji ardhini

Mti huu umetajwa sana kwenye Biblia, Adam na Eva baada ya kula tunda la kati na kujikuta watupu walijisitiri kwa kutumia majani ya mkuyu, Zakayo wakati anataka kumuona yesu alitangulia mbele na kupanda juu ya mkuyu


MBEGU/MAUA



UPANDAJI
Ingawa ni mti mzuri sana kwa wanamazingira lakini ni mti mgumu sana kuuotesha, kuotesha kwa njia ya MBEGU ni ngumu zaidi kwa sababu mbegu zake (ambazo pia ni maua) nyingi huwa tupu ndani bila ile mbegu yenyewe, pia iliziote vizuri ni lazima ziliwe na popo ambao hupenda sana kula matunda yake na kisha ikitolewa kwa njia ya kinyesi ndio inaota vizuri zaidi (seed scarification), mwisho ni lazima ioteshwe sehemu iliyo chepechepe au imwagiliziwe sana.

Njia nyingine ni yakuotesha kwa kutumia matawi yake ambapo unakata na kuyaotesha kama vipandikizi, hii kidogo ina mafanikio lakini ni vipandikizi vichahe tu ndio vyenye uwezo wa kuota na vingi zaidi ya asilimia 90% havioti

9 comments:

Anonymous said...

Mambo Bennet, nimefurahishwa sana nahii blog yako hasa elimu unayotupatia bure. nilikuwa nataka kujua zaidi kuhusu huu mti wa mkuyu maana kuna kisima shambani kwangu lakini wakati wa jua kali huwa kinakauka. nitaupataje na kwa gharama zipi na nitaupanda upande upi wa kisima?

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli elimu nzuri wengi tunafaidika. Asante sana

Bennet said...

Samahani kwa kuchelewa kukujibu ni kwa sababu nilikuwa mashambani si unajua sas hivi ni msimu wa mvua kwa hiyo upandaji unaendelea.

Huu mti ninaweza kukupatia baada ya miezi miwili kwa sababu niliyonayo yote ina order maalum, gharama yake ni sh 10,000 ambapo nitakupa miti miwili

Upande wakupanda mti huu ni upande ulio juu ya kisima kwa sababu maji yanateremka kufuata mteremko na mizizi itafuata mteremko huo huo

Kwa mawasiliano zaidi naomba tuwasiliane kwa emal yangu ambayo ni
mitiki1000@gmail.com

Anonymous said...

Kaka bennet mimi natafuta magome/mizizi ya mikuyu kwa ajili ya dawa naomba unisaidie,napatikana Kinondoni,nitaifuta huko kiluvya kama unayo!!

Bennet said...

Anonymous june 17 naomba uwasiliana nami kupitia mitiki1000@gmail.com niweze kukuletea hiyo mizizi na magamba ya mkuyu

Anonymous said...

Naomba nipatiwe jina la kitaalamu la mti na tunda la komamanga

Bennet said...
This comment has been removed by the author.
Bennet said...

Jina la mkomamanga ni POMEGRANATE na jina la kisayansi ni Punica granatum

Unknown said...

Vipi mizizi yake haiwezi kuharibu kisima kilichojengewa?