KURASA

Saturday, June 13, 2009

MAZIWA YA NGAMIA NA KISUKARI

AINA ZA KISUKARI
Aina ya kwanza ya kisukari ni pale mgonjwa anapohitaji kutumia insulin kila siku, aina hii huwa ni asilimia isiyozidi 10 ya wagonjwa wote wa kisukari, miili yao huzalisha insulin kidogo sana au haizalishi kabisa.Aina ya pili ni ile ambayo mwili mgonjwa wa mgonjwa huzalisha insulin lakini mwili unashindwa kuitumia na baada ya miaka kadhaa mwili hushindwa kuzalisha insulin na kusababisha aina ya kwanza ya kisukari


MDAU AKIMKAMUA NGAMIA


Maziwa ya ngamia yamekuwa yakisifika katika kuwasaidia wagonjwa wa kisukari aina ya kwanza kama watakunywa maziwa haya kiasi cha nusu lita kwa siku. Kwa kawaida mgonjwa wa kisukari aina ya kwanza huitaji kiasi cha ankara 20 za insulin kwa siku lakini akitumia maziwa haya huitaji kiasi cha ankara 6 – 7 za insulin kwa siku.



Huko india katika jimbo la Rajasthan kuna jamii/ kabila linayoitwa Raica ambalo husifika kwa ufugaji wa ngamia, jamii hii husifika kwa kutokuwa na wagonjwa wa kisukari isipokuwa kati ya wale wachache ambao huwa hawatumii kabisa maziwa ya ngamia




Maziwa ya ngamia pia husifika kwa kusaidia wagonjwa wa shinikizo la juu la moyo, pia husaidia katika kupambana na vimelea kama virusi na bakteria. Kwa mfano mgonjwa wa kifua kikuu anayaetumia dawa na maziwa ya ngamia hupata nafuu haraka zaidi ya yule asiyetumia maziwa ya ngamia

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Itabidi tuhamia kwenye nchi hizo wanazofuga Ngamia kama vile Saudi arabia nk. Asante kwa hili, Kaka Benet fungua hospital.

Anonymous said...

mbona sasa hutuwekei posts zinazohusu madawa yatokanayo na miti/matunda/mbegu(natural herbs)nafuatilia karibu kila posts ila sijaona!

chib said...

Nasikia na maziwa ya mbuzi ni dawa! Vipi hayana virutubisho kama ya ngamia?

mumyhery said...

ndugu yangu tupe na maelezo ya ng'ombe na mbuzi kwani hao ni rahisi kupatikana bongo lakini Ngamia tena ndugu yangu huo mtihani

Bennet said...

Aksanteni sana kwa mchango wenu, Anonymous mimi huwa siweki kitu kwa sababu nimesikia au nimesoma sehemu ila ukiona nimeweka kitu ujue nimekifanyia majaribio na nikahakikisha mimi mwenyewe au nimepata maelezo ya kina toka kwa wahusika
Chib ni kweli maziwa ya mbuzi pia ni dawa kama yalivyo ya ngamia sema ya mbuzi hayafikii ubora wa maziwa ya ngamia
Mumyheri naandaa makala kuhusu maziwa ya mbuzi, juzi nilikuwa Kibamba kwa mfugaji mmoja na nikapata maelezo ya kina, nasubiri kuyathibitisha halafu nitachapisha

Anonymous said...

Haya maziwa ya Ngamia hapa Tz Yanapatikana wapi? Mie niko Dar naweza kuyapata pia?

Bennet said...

Anonymous June 23 kama uko Dar nenda ilala mtaa wa Lindi ulizia msikiti wa makuti kuna duka la maziwa utapata maziwa haya

Anonymous said...

Thanks for the info. niko Dar nitaenda kesho jumamosi kuangalia kama ntayakuta!!

Anonymous said...

Thanks Bennet,maziwa niliyapata japo kwa mbinde sana,kuna foleni yaani yanagombaniwa sana.Mungu akubariki sana