KURASA

Monday, December 14, 2009

NDIGANA KALI - EAST COAST FEVER (ECF)

Huu ni ugonjwa wa ng’ombe, nyati na nyati wa India wakaao kwenye maji (water buffalo) ambao umeenea sana hapa nchini kwetu, msambazaji mkuu ni kupe (rephicephalus appendiculatus) na ng’ombe huanza kuugua siku 10 – 25 (wastani siku 14) toka kuambukizwa ugonjwa huu, protozoa aina ya theileria parva ndiye husababisha ugonjwa huu



DALILI KUU ZA NDIGANA KALI
-Joto kali hadi kufikia 42c kwa kawaida ng’ombe huwa na joto 38c
-Manyoya ya mgongoni husimama muda wote na huwa na rangi ya udongo (brown) kwa mbali
-Kuharisha
-Kutoa makamasi laini
-Matezi ya shingo kuvimba
-Kupe aina ya rephicephalus appendiculatus utawaona kwenye masikio ya mnyama (sio lazima)
-Mnyama hushindwa kula vizuri
-Pua (muzzle) huwa kavu bila unyevu unyevu



TIBA
Dawa aina ya BUTALEX ni maarufu sana hapa nchini kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huu, ni muhimu dalili za mwanzo zinapoonekana kumtaarifu mtaalam wa mifugo na ikithibitika ni Ndigana kali tiba ianze mara moja ikiambatana na OTC 20% ili kushusha homa.

KINGA
Kinga kubwa ni kuogesha mifugo yako mara kwa mara, dawa ya ruzuku ijulikana yo kama PARANEX hupatikana katika maduka yote ya kilimo na mifugo. Dawa nyingine nazo zinafaa kuogeshea kwa kufuata masharti ya mtengenezaji.

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa darasa kaka Bennet.

Simon Kitururu said...

Asnte kwa somo Mkuu!

chib said...

Itabidi watu waanze kulipia darasa hili. Nahisi wengi wanachukua notes

Bennet said...

Nawashukuru wote kwa kunitembelea humu, kesho mungu akipenda nitaenda Kisarawe kesho (j5)nategemea kurudi ijumaa asubuhi

Elyc said...

urudipo naomba unielekeze wapi nitapata fresh olive fruits.Sijui kwa kiswahili olive zinaitwaje,i hope utakuwa umenielewa mkuu?

Bennet said...

Elyc ukitaka kupata fresh olive fruits nenda shoprite

Mija Shija Sayi said...

Somo zuri kaka.

Ebenezer Farm said...

Habari za siku Bennet, mimi ni mdau wa siku nyingi kwenye blog hii kwa kweli kuputia hapa nimejifunza na kuanzisha ufugaji mbalimbali. Sasa nimeanza kufuga ngombe, ningependa kuotesha majani yangu nimetafuta mkalianda, mronge na leucaena nimepanda ila majani ya tembo, matete na ukoka kila nnakouliza hawana. Msaada yeyeto anayejua wapi itapata mbegu zake nitanunua na kuyafuata. napenda kufugia ndani kuepuka magonjwa nina 20x20m iko wazi ningepanda haya ili kupunguza gharama ya kununua. Asante