KURASA

Friday, September 17, 2010

SHARK - MKEMIA WA MAJI

Leo nilikuwa nabadili maji kwenye chombo cha kufugia samaki wa urembo (aquarium)baada ya kuweka maji masafi na kuwarudisha samaki wangu kuna kitu nikakigundua. Pamoja ya kwamba samaki wote ni wa urembo lakini kila mmoja anatabia yake, ni samaki wawili aina ya shark ambao wanauwezo wa kutambua maji kama yana kitu chochote kibaya, kwa mfano kama kemikali yoyote, chumvi au madini yoyote yale zaidi ya kiwango cha kawaida. Mara tu utakapowaweka kwenye maji ambayo hayako sawa basi utawaona wanakaa chini tu na wala hawaogelei kama kawaida yao.

Wakati narudishia mawe kwenye chombo chao yalisuguana na chenga chenga zake zikabadili ubora wa maji, ingawa hayakuwa na tatizo lolote kiafya lakini samaki hawa aina ya shark waliweza kugundua hilo na walikaa kama wanavyoonekana hapa kwenye picha mmoja aligeuka juu chini kama vile kafa.Baada ya kuona wako hivo nikawasha pampu ya kuongeza hewa kwenye maji pamoja na filter baada ya dakika kama 10 samaki hao wakaanza kuogelea kama kawaida, angalia video hii


Hawa hapa kwenye video ni goldfish aina ya shubunkin, redcap na goldspike


Angel fish ni aina nyingine ya samaki nilionao


Huyu anajulikana kama catfish, nayeye kazi yake kubwa ni kisafisha vioo na urembo wa ndani, anauwezo pia wa kumla samaki yoyote aliyekufa bila ya wewe kuanza kuhangaika kumtoa

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kumbe hata samaki wana lugha na kaka Bennet unaweza lugha ya samaki. Nilipokuwa mdogo wakati nikiishi Lundo-Nyasa watu walikuwa wanasema ukila kichwa cha samaki basi utakuwa na akili sana... je ni kweli Samaki ana akili sana?

Anonymous said...

shark ni aggressive fish humuwezi kumueka na communty fish cat anggelfish na coldfish ni communty shark anatakiwa awekwe kwenye maji yenye conditions ya maji nyenye temperature 22 -28 degres sababu iliyowafanya shark kukaa chini ni mshtuko na tofauti ya maji unayoweka wakati kwa kubadilisha yale uliyoyatoa yana tofauti ya temperature unayoyaweka ni vizuri kubadilisha maji bila ya kujuwa tiya mpira uyavute na weka mpira kuyaweka kwenye tank bila ya kuwasumbuwa samaki vilevile tofautisha samaki wa tropical na wanaoishi kwenye majii ya baridi kama coldfish

Bennet said...

Dada Yasinta tulipokuwa wadogo tuliambiwa ana akili sana (samaki) sababu ya kuweza kuogelea kwenye maji wakati sisi hatuwezi

Annony unachoongelea kuhusu kwa nini waligeuka na nilichoongelea mimi ni sawa kwa sababu wanatest minerals, PH na temperature ya maji, kuhusu kubadilisha hiyo ya kutoa na kurudishia kwa mpira ni partial water change hufanyika mara 1 kila wiki na kila baada ya wiki 4 inabidi kutoa maji yote (full water change) kama nilivyo fanya mimi, kwangu mimi shark kusense tofauti ya maji si kitu kigeni kwa sababu nimemfuga kwa miaka mingi tu sasa ana ukubwa wa zaidi ya inchi 10+

kuhusu kuchanganya samaki ni muhimu sana kwa sababu kila samaki ana jukumu lake madhali tu wasidhuriane kama kugombana n.k hapo kwangu bado sijaweka zebra ili chombo kitimie

Anonymous said...

mtalam wewe tunakuamini nandiyo tegemeo letu sisi walalahoi nilichangiya mada bila ya kutabua kama wewe ndiye muhusika wa tenk na samaki ok mimi nnalo tank vilevile nnazo aina 7 za shark lakini kutokana na mazingira ninayoisha naweza kukaa muda mrefu bila ya kubadilisha maji kwenye tenk mwaka na zaidi ninachofanya ni kubadilisha filta pale ninapoona kuna mabadiliko ya maji kuhusu PH value between 5.8&7.8 na maji wanapokuwa mazito yanatakiwa DH in 5.0 to 15gange mtalam shark wako wana perfect bodies 10 incher jee anamiaka mingapi?shark wanaishi8to 12year na wanakuwaup 14 inches na kwa 3year ankuwa 25cm mtalam naomba kujuwa bongo wanatatikana piranha fish jee ni mkoa gani au sehemu gani tz mdau wa pangani

Bennet said...

Aksante sana Anony kwa maoni yako, shark si mchafuzi sana wa maji ila hawa gold ni balaa maana wanakula kama nguruwe kila saa ndio maana wanachafua sana tank, tank langu ni lita 220 sasa kuna gold wanne, shark wawili, cat fish mmoja na angels watano, kwa hiyo wanachafua sana, huyu shark ana kama miaka minne au kasoro

kuhusu Piranha sijui wapo wapi bongo, ila ninachojua ni kwamba walipigwa marufuku kusafirishwa duniani kwa sababu ya kutishia uhai wa samaki wengine kwa kuwaua na kuwala