KURASA

Saturday, January 23, 2010

MTI MZEE ZAIDI DUNIANI

Mti mzee kuliko yote duniani ulio hai ni bristlecone pine (Pinus longaeva) unaoitwa Methuselah mti huu unapatikana marekani California katika mlima mweupe, mti huu ambao uko futi 11,000 juu ya usawa wa bahari una miaka 4838 na sio tu ni mti mzee zaidi bali ni kiumbe kizee zaidi duniani cha asili (non-cloned) kilicho hai
Kabla ya Methuselah haujagunduliwa kwamba ni mti mzee zaidi duniani Mwaka 1957 na Edmund Schulman iliaminika kwamba mti mkubwa aina ya Sequoias ndio mti wenye umri mkuwa zaidi ukiwa na miaka 2000

MITI AINA YA METHUSELAH HUKO CALIFORNIA KATIKA MLIMA MWEUPE


Mti mwingine aina ya Prometheus uligunduliaka baada ya mwanafunzi wa Mwaka wa mwisho chuoni 1964 ajulikanaye kama , Donald R. Currey alipokuwa akifanya majaribio ya kisayansi na kifaa chake cha kuchimbia viini vya miti miti kuvunjika ndani ya mti, aliomba ruhusa ya kuukata mti huo (iliauchunguze zaidi) kutoka idara ya misitu na alistaajabu alipokubaliwa (wenzetu hawakati miti hovyo hovyo bila sababu maalum) na baada ya kuukata mti huo ndipo walipogundua kwamba ni mti wenye umri mkubwa zaidi duniani ukiwa na zaidi ya miaka 5000.

MITI AINA YA METHUSELAH WENYE MIAKA 4838



Kwa hiyo Prometheus ndio mti mzee zaidi kugunduliwa lakini umekufa baada ya kukatwa na Methuselah ndio mti mzee zaidi duniani ulio hai mpaka sasa. Miti ya Methuselah iko mingi na yote ikiwa na umri zaidi ya miaka 4000 na ipo California katika mlima mweupe lakini mahali ulipo kutwa mti wa Prometheus pamefanywa siri kwani bado wanaendelea kulichunguza eneo hili wakiamini wataukuta mti mwingine wenye umri unaofanana na ule walioukata

KISIKI CHA MTI WA PROMETHEUS BAADA YA KUKATWA

3 comments:

Elyc said...

good stuff!!!

chib said...

Nafikiri hata ukiingia huko kwenye misitu ya Kongo, kuna uwezekano ukakuta miti iliyoota mpaka na mvi kwa uzee.
Bennet kwa nini usifanye mkakat wa kwenda kuchunguza huko Kongo? Anza kukusanya mahela bwana kwa utafiti huo.
Ni wazo tuuuuu

Bennet said...

Ni kweli maana ukienda moshi kuna mti mkubwa sana ambao watu zaidi ya kumi mkishikana mikono kuuzunguka ndio ukubwa wake, sasa sijajua ni mkubwa sana tu au ndio na umri ni mkubwa pia