KURASA

Friday, March 19, 2010

MBWA WAKIPANDANA KWA NINI HUNASIANA AU KUNATANA?



Nadhani karibia kila mtu ameshawahi kuona mbwa wakipandana, kama bado basi maelezo haya yatakusaidia siku ukiwaona, mara baada ya mbwa dume kumpanda jike utaona dume anageuka na kupeana mgongo na jike kila mmoja akiangalia upande wake wakati huo huo, uume ukiwa bado ndani ya uke, wanakuwa kama wanavutana na wakati mwingine wanaweza kutoa milio kama wanalalamika, unaweza kuhisi wanaumia na ukataka kuwatenganisha ACHA na wala usijaribu kufanya hivyo utawaumiza.

Kwa kawaida mbwa dume anapoanza kumpanda jike uume unakuwa haujasimama bali husaidiwa na kiuongo kijulikanacho kama baculum, hii ni tishu kama mfupa na iko ndani ya uume wa mbwa. Wakati mbwa dume anapotaka kumwaga manii ndani ya uke ndipo damu hujaa kwenye uume na hapo uume hutanuka (kudinda) kwa hiyo akimaliza kutoa manii uume hunasa ndani ya uke kwa sababu ya kule kutanuka.



Mbwa dume anapogeuka anazipa muda Mbegu za kiume ziweze kuingia vizuri kwenye uke na hivyo kusababisha ujauzito, ukitumia nguvu kuwaachanisha, mbali na kuumia pia jike hataweza kupata ujauzito. Hiki ni kitu cha asili kwa hiyo husaidia pia kuzuia madume mengine yasiingilie tendo hili na kulikatisha wakati Mbegu bado zinaogelea na kuyafuata mayai kwenye mji wa mimba, kwa kawaida hata kama mbwa madume walikuwa wanapigana kila mmoja akitaka kumpanda jike, mara baada ya Yule aliyefanikiwa kupanda na kugeuka wale wengine huacha vurugu zote.

MBWA WALIONASIANA BAADA YA KUPANDANA


Tendo hili huchukua kati ya dakika 20 – 30 na mbwa hufanikiwa kunasuka mara baada ya damu kupungua kwenye uume na uume kusinyaa na kupungua ukubwa. Kwa mbwa dume ambaye ni mara yake ya kwanza kupanda basin a hata yeye huchanganyikiwa atakapoona amenasa, anaweza hata kujaribu kujinasua au kupiga kelele, unachotakiwa ni kumshika shika shika mbwa wako kichani huku ukimuongelesha kwa upole, yaani jaribu kumpunguza presha ili atulie

17 comments:

chib said...

Nani huwa anakaa karibu na mbwa wanapokuwa kwenye kipindi joto!
Tena ndo ije ya kumshikashika kichwa he heeh hee

Faith S Hilary said...

Wow! This is so interesting, I never knew! Asante kwa infomation nzuri kabisa kaka, you have opened my eyes.

Mbele said...

Candy1, hii habari inanikumbusha nilipokuwa mtoto, kijijini. Wavulana tulikuwa tukishawaona mbwa namna hii, tunatafuta mawe na vipande vya matofali na kuanza kuwafukuza na kuwapiga.

Tulikuwa tunaona burudani sana kuwarushia hayo mawe na vipande vya matofali. Hatukuwa na sinema au disco kijijini, kwa hivi, kama si kuchunga mbuzi na ngombe, burudani zetu zilikuwa ni hizo, pamoja na kufukuza panzi, ndege, na kadhalika.

Yaani nikikumbuka tulivyokuwa tunafanya, sijui najisikiaje, maana ni ukatili wa hali ya juu, lakini hatukuwa tunawaza hivyo.

Simon Kitururu said...

Umenikumbusha mbali sana Mkuu!

Anonymous said...

je mbwa aliyehasiwa anauwezo wa kutenda tendo hilo.au anakuwa hana uwezo wa kupanda jike tena. tendo la maramoja mbwa anapata bimba au mpaka warudie mara nyingi?

Bennet said...

mbwa aliyehasiwa hawezi kupanda wala kutenda tendo hili, ila wivu wa mapenzi anakuwa nao kama kawaida, ukitaka aendelee kupanda bila kuzalisha unamfanyia vasektomi

Mbwa akipandwa mara moja anaweza kupata mimba ila atazaa watoto wachache au hata mmoja ila anatakiwa arudie kwa siku 3 - 7 kutegemeana na breed ya mbwa mwenyewe, kila siku kuna mayai mapya yanazalishwa

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

duh! kaazi kweli kweli!

Israel Saria said...

Benet hebu tupe ya Nguruwe.Nikiwa chuoni Tengeru tulikuwa na mwalimu mmoja anaitwa Mushi. yeye alikuwa anatuonyesha kwa mfano na kupelekea hata nguruwe kupoteza fahamu na hata kuhitajika kumwagiwa maji ili kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya tendo la kujamiana.

Sparrow David said...

Na mbwa anahasiwa vip?

Sparrow David said...

Na mbwa anahasiwa vip?

Unknown said...

Hivi akipandwa na mbwa wawili tofauti na siku tofauti halo nitegee kupata mbegu ya mbwa wa kwnza au wapili

Unknown said...

0787551211 whsp

passionfleva said...

Kwa Mara ya kwanza umbwa jike anaingia kwenye joto akiwa na umri gani

POZ group LTD. said...

Ivi naweza kuchukua mbegu za mnyama mwingine nkapandisha kwa mbwa?

Davies said...

Chakula gani kizuri kwa mbwa hasa baada ya kujamiiana?

Chiza onesmo said...

Ok iyo nimeisoma

Unknown said...

Hatari