KURASA

Thursday, May 27, 2010

BIO -GAS / HEWA VUNDE

Kuni na mkaa vimekuwa vikiongezeka bei kila siku pia vikiwa ni vyanzo vya uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji miti, njia mbadala inahitajika katika kutatua tatizo hili kwa wakulima, na kinyesi cha wanyama kinaweza kutumia kuzalisha nishati ijulikanayo kama BIO –GAS

Kinachofanyika ni kukusanya kinyesi cha wanyama hasa ng’ombe wanaofugwa ndani, kikichanganyika na mkojo pamoja na maji yanaelekezwa katika tanki maalum kwa ajili ya kuzalisha nishati hii. Baada ya bacteria kuozesha mchanganyiko huu kwa njia isiyohitaji hewa ya oksijeni (anaerobic fermentation) nishati ya bio gas huzalisha ikiwa na wastani wa hewa ya METHANE 65% na kasha gasi hii huelekezwa kwenye nyumba kwa kutumia mabomba hadi jikoni kwa ajili ya kupikia

Mchanganyiko uliokwisha tumika hutoka nje wenyewe kwa kusukumwa na mchanganyi ko mpya mara uingiapo, kinyeshi kinachotoka nacho pia hutumika kama mbolea kwa ajili ya kustawisha mazao ya mkulimaFAIDA ZA BIO-GAS
1-Huongeza kipato cha mkulima kwa kupunguza muda wa kutafuta kuni na mkaa

2-Husaidia katika utunzaji wa mazingira kwa sababu haichafui hewa na hupunguza ukataji miti hovyo

3-inaweza kutumika kuwashia taa kama itazalishwa ya kutosha

4-mbolea inayobaki hutumika kwa ajili ya kustawisha mazao

5-Afya ya mkulima hulindwa kwa sababu upikaji kwa kutumia bio gas hauna moshi, kina mama jikoni hawaathiriki na moshi kama wakitumia kuni, badala ya kinyesi cha wanyama kuwa kingi na kukosa matumizi na kugeuka uchafu sasa kitatumika kuzalisha nishati hii

3 comments:

Anonymous said...

We jamaa ni noma maana naona umekamilika kila idara ya mkulima, hongera sana

Albert Paul said...

Kaka Bennet, nashukuru kwa elimu hii nzuri.

Kwa wastani, mfumo huu mzima unaweza kugharimu kiasi gani cha fedha? Bila shaka, wataalamu wanatakiwa, katika eneo langu nitawezaje kuwapata wataalamu?
Nashukuru ndugu Bennet.

Anonymous said...

Shukrani kwa kunifungua macho.
Swali dogo,
Wanahitajika ngombe wangapi ili kupata gesi ya kukidhi mahitaji ya familia ya watu wanne?
Natanguliza shukrani.

PKaberwa