KURASA

Thursday, September 23, 2010

DADA NAYMA ANAOMBA USHAURI ZAIDI

Hello Bro Bennet. Angalia miche yangu hatua iliyofikia bado sijaipeleka shambani,
naomba ushauri zaidi niliiotesha mwezi wa tano mwezi wa saba nikaiweka kwenye mifuko miche 300 tu.
nayma





Dada Nayma leo naomba nikuweke hadharani, wadau huyu dada nimekuwa nikimshauri kuanzia kuandaa mbegu, kitalu, kusia mbegu, umwagiliaji, kuhamisha mbegu kutoka kwenye kitalu hadi kwenye vipakti

Dada Nayma miche yako bado ni michanga kiasi, na kama unafuatilia utabiri wa mvua za msimu wa September mpaka November ni kwamba hakutakuwa na mvua za kutosha ila kwa mikoa ya kanda ya ziwa na zaidi Bukoba, nakushauri endelea kumwagilia miche yako ikue zaidi huku ukisubiri mvua za mwezi wa December mwishoni na January 2011, hapo itakuwa mikubwa ya kuweza kuhimili kama mvua zitakuwa chache

NB Hongera sana na anza kuandaa mbegu nyingine ili mwezi wa January uwe na miche mingi zaidi

5 comments:

Anonymous said...

Hongera Dada Naymah huu ni mwanzo mzuri endelea kupata ushauri kutoka kwa mtaalam, Bennet haya ni mazao ya blog yako, je una wakulima wangapi ambao unawapa ushauri wako wa kitaalam, blog hii ilianza lini na inamuda gani?

chib said...

Pale utakapotaka kuuza iliyokomaa, wanunuzi tupo :-)

Bennet said...

Anony ni kwamba kuna watu wengi ambao ninawapa ushauri wakiwemo baadhi ya viongozi wa serikali ambao wana mashamba makubwa sana, na wanafaidika na kile kidogo ninachofahamu, kuhusu blog hii ilianza mwezi wa tano mwaka 2006, wakati huo bloggers tulikuwa wachache

Salua/Nayma said...

Asante sana Kaka Bennet ujue unafanya kazi ambayo itakumbukwa sana na sisi wakulima chipukizi tunaotaka kujifunza kutoka kwako. Nashukuru kwa ushauri wako nitaufanyia kazi ila jana nimeshakabidhiwa kisima changu kwa ajili ya kumwagilia endapo nitakosa mvua na kipindi cha kiangazi. Chib nina miche mingi ambayo ninaikuza bado mingine waliniomba marafiki nikawaeleza sitawapa bure ili wawe na uchungu nayo wakikumbuka gharama waweze kuikuza. Naamini nitaipeleka shambani kipindi nitakapoona mvua za kutosha zimeshaanza. Asante kwa blog hii kwa mafunzo mengi kwa wakulima.

Anonymous said...

samahani kaka labda ungetuwekea wazi mfumo mzima wa utayarisharishaji mbegu, kwasisi wakulima chipkiz unatutesa na washauri ni wengi, nashukuru kwa kujitolea kutusaidia Mungu akibariki.