KURASA

Friday, January 7, 2011

KAMPUNI YAINGIZA MIKARATUSI YENYE UGONJWA SERENGETI

Kampuni ya tumbaku ijulikanayo kama Alliance One Tobacco imeingiza miche ya mikaratusi toka nchini Kenya yenye Magonjwa na kuisambaza kwa wakulima wilayani Serengeti.

Magonjwa hayo ni ugonjwa wa kukauka miche pamoja na ugonjwa wa mizizi (Eucalyptus root disease)imebainika na wataalamu toka maabara ya Chuo kikuu cha Sokoine (Morogoro) kwamba magonjwa hayo hayatibiki, ila ugonjwa unaweza kudhibitiwa kabla haujaibuka kwa kupiga dawa iana ya Acephate au Confidor wakati miche ipo kitaluni kabla ya kupandwa shambani.



Kitaalamu nashauri kabla ya kuingiza mbegu au miche ni lazima uchunguzi ukafanyika kwa kina ili kugundua kama kuna magonjwa ambukizi, kwa sababu kuna aina zaidi ya 200 za mikaratusi

kwa ushauri zaidi kwa mtu anayetaka miche au mbegu za miti, basi awasailianae na wakala wa mbegu za miti wa taifa (TTSA) ambao wapo Morogoro eneo la kihonda, pamoja na hayo baadhi ya tafiti zimeonyesha kwamba mikaratusi inaathari kwa mazingira kwa sababu inatumia kiasi kikubwa cha maji na kusababisha ukame hasa kipindi hiki cha mabadiliko katika tabia nchi



WITO sehemu kama serengeti ambapo ni urithi wa dunia nashauri makampuni na watu binafsi wajitahidi kupanda miti ya asili na kuachana na hii miti ya kigeni kama mikaratusi, sijaelewa pia kwa nini miti itoke nchi jirani ya Kenya wakati wangeweza kuanzisha vitalu hapa hapa nchini kwa kutumia mbegu ambazo tunazo tena za miti ya asili

6 comments:

chib said...

Awali ya yote, Napenda nikupe heri ya mwaka mpya

Unknown said...

Heri ya mwaka mpya mkuu. Labda tungepewa jibu na wahusika kwamba ni kwanini miti itoke Kenya ilhali uwezo wa kuwa na vitalu vyetu tunao? Swali lingine ni kampuni ya tumbaku ya kigeni inafanya nini Seerengeti?

emu-three said...

Au ndio mbinu za kibiashara, kuingiza miti yenye ugonjwa ili ituangamizie miti yetu ya asili?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nataka elimu juu ya kilimo cha vitunguu mkuu!

Nayma said...

Kamala Hapo juu kwenye picha ya kaka Nennet pana dirisha limeandikwa tafuta kwenye blog hii andika neno vitunguu itakuletea topic hiyo utajifunza hapo.

michael gomela said...

Nadhani kuna haja ya kuchukuwa sheria mkononi kuikata hii mti ya mikaratusi kama mbao mbona miti mingi sana nyumbani, kwanini tunangangania hii mti mibaya kabisa kwa mazingira yetu na vilembwe wetu?