KURASA

Wednesday, September 28, 2011

WILAYA ZA NGORONGORO NA LONGIDO ZAKUMBWA NA UGONJWA HATARI WA HOMA YA MAPAFU YA NGOMBE



Wilaya za Ngorongoro na Longido ambazo zipo mpakani na Kenya zimekumbwa na ugonjwa wa mapafu wa ng'ombe, hali hii imefanya jumla ya ng'ombe milioni moja (1,000,000) kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu.

Ugonjwa huu ulitangazwa kama janga la kitaifa mnamo mwaka 2001 kwa sababau ni hatari sana na unaua ng'ombe kwa kasi sana, na unaweza kudhibitiwa kwa kuchanja mifugo mara unapoonyesha dalili za mlipuko.

Kutokana na hilo serekali imechukua hatua za dharura za kuwachanja ng'ombe wote katika wilaya ya Ngorongoro, Longido na zile za jirani kama Karatu na nyinginezo.

Historia ya ugonjwa huu inaanzia enzi za ukoloni mnamo mwaka 1905 na uliweza kudhibitiwa, lakini mnamo mwaka 1964 mwaka ambao ndio wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokea na Tanzania kuzaliwa, ugonjwa huu ulilipuka tena nchini mwetu. mnamo mwaka 1990 ugonjwa huu ulilipuka tena katika Wilaya ya Loliondo mpakani na Kenya.



Mwaka 1994 ugonjwa huu ulilipuka tena na kusambaa hadi mkoa wa Morogoro katika wilaya za kilosa na Mahenge. na mwaka 1998 ugonjwa huu ulisambaa katika mikoa 11 ya nchi yetu

Ugonjwa huu hujulikana kama contagious bovine pleural pneumonia au CBPP kwa kifupi na kama unataka mifugo yako ichanjwe wasiliana na maofisa ugani waliokaribu nawe au ofisi za wizara ya mifugo

No comments: