Wakati leo tunaazimisha siku ya kichaa cha mbwa duniani, ugonjwa huu hapa nchini kwetu bado umekuwa tatizo sugu. Katika wilaya ya Temeke pekee watu 202 waling'atwa na kati ya hao 19 waliugua kichaa cha mbwa. Wilaya hii inajumla ya mbwa 4500, paka 1500 ambapo kati ya hao 3418 walifanikiwa kuchanjwa.
CHANJO YA KICHAA CHA MBWA (RABIES) KWA AJILI YA WANYAMA
Ugonjwa huu huweza kumpata viumbe vingi ikiwemo binadamu, ng'ombe, mbuzi, kondoo na kadhalika, na wasmbazaji wakuu wakiwa mbwa na paka ingwa kuna baadhi ya poo (vampire bats) nao pia husambaza ugonjwa huu kwa kung'ata na kusambaza vimelea vya kichaa cha mbwa.
ugonjwa huu upo kila sehemu ya dunia ambapo kwa mwaka huua jumla ya watu 55,000 kote duniani ambapo Afrika watu 21,000 hufa kila mwana na wengine 34,000 hufa barani Asia na kwingineko
Kauli mbiu ya mwaka huu ni TUSHIRIKIANE KUFANYA KICHAA CHA MBWA KUWA HISTORIA na njia pekee ni kuwachanja wanyama wetu, na pia kuwazuia wasizurure hovyo mitaani, MUONE MTAALAM WA MIFUGO ALIYE KARIBU NAWE ILI MBWA NA PAKA WAKO WAPATE CHANJO KAMILI
3 comments:
"na pia kuwazuia wasizurure hovyo mitaani, MUONE MTAALAM WA MIFUGO ALIYE KARIBU NAWE ILI MBWA NA PAKA WAKO WAPATE CHANJO KAMILI" hili ni MUHIMU SANA lakini kuna wengi hawazingatii.
Duh ! Nakumbuka sindano mpaka leo za nilipoumwa na mbwa kichaa nikitoka shule ya vidudu enzi hizo!:-(
DUH! Ila siku hizi kila siku ni siku ya kitu fulani mpaka unawez kuchanganyikiwa Mtu!
Mbwa wasiowezeshwa kimaisha ni hatari sana katika jamii yetu ya Uswazi.
Post a Comment