KURASA

Monday, November 7, 2011

MPWAPWA BREED - Mbegu bora ya ng'ombe iliyosahaulika

ASILI
Mbegu hii inatokana na mchanganyiko wa mbegu ya ng’ombe jike aina ya Zebu toka Tanzania na Red madume ya Sindhi na Sahiwal wenye asili ya india na Pakistan lakini waliotolewa nchini Kenya hii ilikuwa ni mwaka 1940 ambapo uzalishaji wa mbegu hii ulifanyika kwa mara ya kwanza katika kituo cha utafiti wa mifugo Mpwapwa Dodoma nchini Tanzania

Mwaka 1958 uboreshaji wa mbegu hii ulifanyika kwa kuongezea damu za ng’ombe wa ulaya (Bos Taurus) aina ya Ayshire na Jersey na mpaka kufikia mwaka 1960 mbegu ya Mpwapwa ikawa na na uwiano wa 20% Tanganyika Zebu 10% Boran 5% Ankole 55% Red Sindhi na Sahiwal na 10% Ayshire na Jersey. Mpaka mwaka 1971 mbegu hii ikawa na mchanganyiko wa 32% Red Sindhi, 30% Sahiwal, 19% Tanganyika Zebu 10% Boran na 10% Ayshire na Shorthorn, utagundua kwamba mbegu ya Jersey iliondolewa na kuingizwa short horn

MWONEKANO
Wanaonekana zaidi kama Sahiwal wakiwa na rangi nyekundu iliyofubaa mpaka kukooza sana au Nyekundu na nyeupe, Wana nundu kama ng’ombe wetu wa kienyeji, ngozi ya chini yashingo ijulikanayo kama DEWLAP ni ndogo zaidi ya Zebu lakini kubwa zaidi ya Ng’ombe wa kigeni, wana kiwele kikubwa zaidi ya ngombe wa kienyeji chenye kukamilika kirahisi ANGALIZO nundu na dewlap huwasaidia kupambana na mazingira ya Afrika hasa joto kali

MBEGU YA MPWAPWA


Madume yana uzito kati ya kilo 450 – 600 na majike kilo 275 – 300 wakati wa uzazi wa kwanza na huongezeka hadi kufikia kilo 450 hapo baadae, mbegu hii inauezo wa kuzalisha maziwa mengi kuliko ng’ombe wa kienyeji na pia uhimili mazingira ya joto na magonjwa kuliko Tanganyika Zebu

Serekali imeshindwa kusambaza mbegu hii kwa wafugaji na inasemekena karibia itapotea kwa sababu ng’ombe wa Mpwapwa waliobakia ni wachache sana na wanapatikana kwenye baadhi ya vituo vya utafiki kama Mpwapwa kwenyewe. Pia kuna tetesi kwamba kwa sasa hakuna MBEGU HALISI (pure breed) ya ng’ombe hawa kutokana na kuachwa wakapandana ndugu kwa ndugu (Inbreeding)

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni habari nzuri na mbaya je mwisho wake inawezekana tusiwe na aina hii ya ngómbe?

Anonymous said...

ndugu yetu unapotea sana au ndo ubusy na kazi?...wapenzi wako tunategemea kujifunza toka kwako mambo mengi lakini unapokuwa unapotea sana hivyo bila taarifa tunakata tamaa ya kutembelea blog yako...