KURASA

Tuesday, July 30, 2013

KILIMO BORA CHA MANANASI

Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara, Lindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam

HALI YA HEWA
Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 - 32, huwa haya stahimili baridi

UDONGO
Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako.

MSIMU
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.

UPANDAJI
Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90

Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi

MBOLEA
Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

WADUDU
Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.

Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides)kabla ya kupandwa shambani

UVUNAJI
Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi 18  mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji  hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili


3 comments:

Amba said...

Asante sana kwa taarifa nzuri,fupi.Ni wapi Mkuranga au Bagamoyo ambapo naweza kupata miche 100,000 ya minanasi kwa ajiliya kupanda kwenya eka 10?

Hamisi Mhenwa said...

Nimeipenda hiyo elimu ila nahitaji kupanda hiyo mananasi mkoa wa singida wenye ukame kiasi Je, inawezekana?

Unknown said...

Jamani naweza pata mbegu za nanasi niko lindi