KURASA

Tuesday, April 29, 2014

UANDAAJI WA MBEGU ZA MITIKI


 Mbegu za mitiki ni lazima ziandaliwe kabla ya kusia kitaluni, hakikisha umeshaanda kitalu chako mapema na kiwe na udongo wenye rutuba ya kutosha, mwagia maji ya kutosha ili kama kuna magugu yaanze kuota na kung'olewa mapema, hii inasaidia kwa sababu mbegu za mitiki huchukua muda mrefu kuota, sasa ukianza kung'olea na mbegu hazijaota au miche ni midogo utakuwa unaing'oa na yenyewe


 Kwa kila kilo moja ya mbegu ina hitaji ndoo ya maji lita 20, weka mbegu zako kwenye gunia au kiroba, kisha weka vitu vizito kama mawe ili kuhakikisha mbegu zako zinakuwa chini ya maji, kinyume na hapo zitaelea juu na hutapata matokeo mazuri katika uotaji, bila kufanya hivi mbegu zko hazitaota kwa wingi

 Hili ni pipa la lita 200, linatosha kwa kilo 10, badilisha maji yako kila jioni na asubuhi kwa muda wa siku 7. kama utaweka maji mara mbili zaidi unaweza kubadilisha maji mara moja kwa siku, yaani kilo moja kwa maji lita 40. Kama kuna maji yanayotembea kama vijito vidogo basi unaweza kuloweka humo bila kuziondoa kwa siku 7.

 Siku ya 8 anika mbegu zako juani, ni vizuri kama utaziweka kwenye bati ili zipasuke gamba lake na kusaidia uotaji

 Panda mbegu zako kwa msitari, chora mfereji wenye kina cha sentimeta moja na uziweke kwenye huo mfereji mwanzo mpaka mwisho bila kuruka nafasi, acha nafasi ya sentimeta 18 - 20 kati ya fereji na mfereji kama inavyoonekena kwenye picha juu na chini


Baada ya wiki tatu mbegu zitaanza kuota na zitaacha kuota baada ya siku 65, uotaji ni kiasi cha  45% mpaka 50%, kilo moja ina wastani wa mbegu 800 mpaka 1000, kwa hiyo unaweza kupata mpaka miche 500 kwa kilo moja, Mbegu zinapatika kwa WAKALA WA MBEGU WA TAIFA kwa bei ya shilingi 9000/= kwa kilo, wanapatikana Morogoro mjini, eneo la Kihonda ukitokea msamvu kama unaelekea Dodoma ni kama kilometa 3, unaweza kupanda daladala, bodaboda au hata taxi na ukafika
9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimefurahi kupata hili soma la mitiki..Maana nilipanda mitiki miaka 6 iliyopita nikienda tena nitaikuta mikubwa na nadhani nitakuhitaji/hitaji ushauri wako..Ahsante sana

Bennet said...

Hili somo nilishalitoa nyuma ila watu hawataki kutumia sehemu ya search, nitumie mail dada Yasinta

Rick John said...

Ebana broh niaje niaje .... nataka kupanda hii miti na nahitaji kupata mafunzo zaidi ili niweze kufanikisha hili suala langu na miche tayari ninayo .....
help me please #

mick said...

Asante sana kwa moyo wako wa kutaka kuwakomboa watu katika maisha ya utegemezi wa ajira hapa kwetu tanzania,nimependa kutuatilia mjadala hii wenye mwelekeo chanya hasa katika uwekezazi katika sekta ya kilimo,mimi pia nimevutiwa katika kufanya kilimo hata kwa ajiri ya biashara,nimejaribu kufuatilia na kikaona kilimo cha zao la mbao ninafaa sana kwa ajiri ya baadae.Hivyo naomba kujua ni maeneo gani yanafaaa kwa kilimo cha MITIKI, na ni kwa muda yani naweza kupanda mpaka kuvuna..Asante

ChalaInvestment.com said...

Ndugu asante kwa somo zuri ila nahitaji msaada kuhusu upandaji wa mitiki maeneo ya pwani. Je? Inaweza kustawi maana shamba langu lipo Kibiti. Asante sana

kighi said...

Habari za leo wadau, nami pia nimevutiwa na kilimo hiki cha miti ya mitiki jamani, naomba kupata ushauri kitalaamu kama eneo la Korogwe linafaa maana nina shamba pale, na pia naomba kama una shamba linafaa kwa kilimo cha mitiki nambie ni bei gani na ni wapi

athumani mauridi said...

ahasante kaka kwa somo, mimi nimenza hatua ya kwanza kaka leo, je naweza kupanda mbegu moja kwa moja kwenye viriba badala ya kuandaa kitalu?

KAWINGA jr said...

Shariphkawinga1@gmail.com

Martin Malecela said...

Asante